51109 Street, Tumaini, Iringa Mon-Sat 09am-5pm, Sun Closed
Call Now
+255 741 614 903
STAR OF NEW GENERATION1
Mail Now
info@sng1.co.tz
Star of New Generation1 Company Ltd — Huduma Zetu
FURAHIA HUDUMA ZETU

Afya ya Akili
kwa Ustawi Wako

Star of New Generation1 Company Ltd ni kampuni pekee inayokupatia huduma bora za Afya ya Akili kwa ustawi wako na hata vizazi baada yako. Karibu ufahamu zaidi kuhusu PACKAGES za huduma zetu.

Chagua Package →
"AFYA YA AKILI KWA USTAWI WAKO NA VIZAZI BAADA YAKO"

Star of New Generation1 Company Ltd

Kampuni ya kwanza Tanzania, Afrika na duniani inayojikita kwenye afya ya akili.

Kuhusu SNG1

Star of New Generation1 Company Limited (SNG1) ni kampuni ya kwanza Tanzania, Afrika na duniani inayojikita kwenye afya ya akili inayolenga ustawi wa mtu na vizazi kupitia matumizi ya kutambua uwezo unaoacha alama. SNG1 ni kampuni inayotambulika na kusajiliwa rasmi nchini Tanzania ikiwa na namba ya usajili 171466490. Malengo ya kampuni hii ni kuhamasisha na kuleta chachu ya mabadiliko ya kifikra kwa watu wote kuwa tayari kutambua, kukubali, kudhihirisha, kutathimini na kuwa na mwendelezo wa matumizi sahihi ya uwezo walionao.

Namba ya Usajili: 171466490

Mwanzilishi

SNG1 ilianzishwa na mtaalamu na mbobezi wa saikolojia, Baraka T. Adolph Mushobozi mwaka 2021, na ilianza kama ofisi. Kama mwanzilishi, mwanasaikolojia Mushobozi ni mtaalamu wa kutoa huduma za kisaikolojia na huduma zinazohusiana na maabara ya saikolojia. Pia, anatoa mafunzo ya kujengewa uwezo na kuimarishwa kimbinu kwa watu binafsi na wataalamu ndani ya Tanzania na kutoka mataifa mbalimbali duniani. Mushobozi amefanikiwa kuunda na kuandika 'psychological models' zinazosaidia kuongoza utoaji wa huduma za kisaikolojia kupitia SNG1 na taasisi nyingine zinazotoa huduma za kisaikolojia.

“AFYA YA AKILI KWA USTAWI WAKO NA VIZAZI BAADA YAKO”

Chagua Package

Inayokufaa zaidi na ufurahie maisha yako ukiwa na Afya bora ya Akili kwa Ustawi wako na vizazi baada yako.

Packages Zetu

Tazama maelezo ya kina, faida na wanufaika wa kila huduma.

Career Visionary

Taaluma
“Jenga msingi imara wa safari yako ya Kitaaluma”
Career Visionary
Maelezo

Huduma hii inalenga kuwasaidia watu binafsi, makundi, na taasisi za kielimu kupata mwongozo wa kisaikolojia kuhusu mwelekeo wa taaluma zao. Tunatoa msaada wa kitaalamu ili kuwasaidia kuchagua njia na maamuzi sahihi ya taaluma/kazi, na kupata mafanikio kwenye maisha ya kazi.

Wanufaika: Wanafunzi, wafanyakazi, vikundi, taasisi za elimu, makampuni, wazazi, na watu binafsi wanaotaka kuongeza ufanisi na mafanikio kwenye taaluma zao.
Faida za Huduma hii
  • Utapata elimu ya kina kuhusu chaguo lako la taaluma (career choice)
  • Utapata mwongozo wa kitaalamu ili kuchagua na kusimamia mwelekeo sahihi wa taaluma unayotaka
  • Vipimo vya kisaikolojia na msaada wa kitaalamu kwaajili ya kuimarisha utendaji wako wa kazi
  • Utapata ushauri wa jinsi ya kuongeza ufanisi kazini kupitia vipimo maalumu vya kisaikolojia
  • Utapata Kozi za kujengewa uwezo na kuimarishwa kimbinu (Mentorship na Coaching) zinazosaidia kukuza uwezo wa kitaaluma na ustawi wa kiakili
  • Utafaidika zaidi na kufahamu saikolojia ya kuishi taaluma yako pendwa

Star Waridi

Uzalishaji
“Zalisha kwa ufanisi zaidi, ongeza tija kwako binafsi na timu yako”
Star Waridi
Maelezo

Huduma hii inalenga kuwasaidia watu binafsi, vikundi, mashirika na viwanda kuelewa jinsi afya ya akili inavyoathiri uzalishaji. Kwa kutumia mbinu za kisaikolojia, tunatoa msaada wa kuimarisha, kuongeza na kufikia malengo ya uzalishaji kwa ufanisi mkubwa.

Wanufaika: Wafanyakazi, vikundi, makampuni, viwanda, taasisi, na watu binafsi wanaotaka kuongeza na kuimarisha ufanisi wa uzalishaji na kuboresha matokeo yao kazini.
Faida za Huduma hii
  • Utapata uelewa wa jinsi afya ya akili inavyoathiri uzalishaji
  • Mwongozo wa jinsi magonjwa ya kisaikolojia yanavyoathiri uzalishaji kazini
  • Utajifunza namna ya kudhibiti msongo wa mawazo kazini na kuongeza ufanisi na tija kwako binafsi
  • Utapata vipimo vya kisaikolojia na matibabu ya kuboresha uzalishaji kazini
  • Utapata mafunzo ya namna fikra ya vizazi (generational mindset) inavyoweza kuongeza tija kazini
  • Ufanisi wa kuzalisha kupitia mwongozo wa kipekee wa uzalishaji wenye afya ya akili thabiti

Star Bahari

Mahusiano
“Boresha mahusiano yako ili kudumisha furaha, amani ya moyo, pamoja na ustawi wako na vizazi baada yako”
Star Bahari
Maelezo

Package hii hujumuisha huduma zinazolenga kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watu binafsi, wenza, na wanandoa ili kuboresha afya ya akili katika mahusiano yao. Kwa kuzingatia changamoto mbalimbali za mahusiano, tunatoa ushauri na matibabu ya kisaikolojia ili kujenga misingi imara ya uhusiano wenye afya.

Wanufaika: Watu binafsi, wenza, wanandoa, familia, na vikundi vinavyohitaji msaada wa kisaikolojia katika mahusiano yao.
Faida za Huduma hii
  • Utajifunza ujuzi na namna bora ya kujitambua na kudhibiti hisia zako
  • Utapata ushauri wa kisaikolojia kwaajili ya mahusiano kabla ya ndoa na ndoa yenyewe
  • Vipimo na tiba ya kisaikolojia katika kushughulikia makovu ya kihisia na kuimarisha uhusiano wako
  • Utajifunza namna mabadiliko ya kifikra na mtazamo yanavyoweza kuimarisha uhusiano wako na kizazi chako
  • Utapata ujuzi wa jinsi magonjwa ya kisaikolojia yanavyoathiri mahusiano na namna ya kukabiliana nayo
  • Utapata mafunzo juu ya jinsi ya kudhibiti msongo wa mawazo au sonona inayotokana na changamoto za mahusiano

Star Talk

Ushauri Nasihi
“Karibu usikilizwe, tuzungumze na upate msaada wa kisaikolojia pia”
Star Talk
Maelezo

Package hii hujumuisha huduma zinazolenga kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa watu binafsi na makundi kulingana na changamoto zao. Tunatoa huduma za kitaalamu kwa kutumia mbinu mbalimbali za unasihi ili kujitambua, kudumisha ustawi wa akili na kuboresha uwezo wako wa kukabiliana na changamoto za maisha.

Wanufaika: Watu binafsi, makundi, wanafamilia, wanafunzi, wafanyakazi, taasisi, na watu wote wanaohitaji ushauri na msaada wa kisaikolojia.
Faida za Huduma hii
  • Utapata nafasi ya kuzungumza na kujadili kwa pamoja juu ya changamoto zinazokukabili
  • Utapata ushauri wa kitaalamu kuhusu changamoto zako za maisha
  • Utafaidika na darasa maalumu la kujitambua na kujua uwezo wako wa kukabiliana na changamoto
  • Utanufaika na mafunzo maalumu na ujuzi thabiti wa kukabiliana na matatizo na changamoto za afya ya akili
  • Utapata vipimo vya kisaikolojia kwaajili ya kutathimini na kupata ufumbuzi wa changamoto zinazokukabili

Star Nest

Familia
“Familia ndio msingi bora wa ustawi wako na vizazi baada yako”
Star Nest
Maelezo

Ndani ya Package hii, utapata huduma zinazolenga kutoa msaada wa kisaikolojia kwa familia zinazokabiliwa na changamoto mbalimbali. Tunatoa huduma za kipekee za kisaikolojia ili kuboresha ustawi wa familia kwa faida ya kizazi cha leo na vizazi vinavyokuja, huku tukizingatia afya bora ya akili katika kila hatua ya mzunguko wa maisha ndani ya familia.

Wanufaika: Familia, wanandoa, wazazi, watoto, na jamii zinazohitaji msaada wa kisaikolojia kwa ustawi wa familia zao.
Faida za Huduma hii
  • Familia itapata elimu kuhusu namna mzunguko wa maisha ya familia unavyoathiri afya ya akili
  • Ushauri wa jinsi ya kudhibiti matatizo ya familia na kuboresha uhusiano ndani ya familia
  • Matibabu na vipimo vya kisaikolojia kwa familia zenye changamoto za afya ya akili
  • Mafunzo na ujuzi wa namna msongo wa mawazo na magonjwa ya akili yanavyoathiri ustawi wa familia na jinsi ya kukabiliana nayo
  • Mafunzo na ujuzi thabiti wa kudhibiti migogoro na athari zake ndani ya familia na hivyo kuimarisha afya ya akili kwaajili ya kudumisha familia zenye furaha

Strawberry Star

Vipaji
“Tambua na tumia vipaji vyako kwa ustawi wa mafanikio yako na vizazi baada yako”
Strawberry Star
Maelezo

Package ya Strawberry Star inalenga kuwasaidia watu binafsi kutambua, kukubali, na kutumia vipaji walivyonavyo ili kujenga maisha bora. Tunatoa msaada wa kisaikolojia na mwongozo kwa watu binafsi kutumia vipaji vyao kwa ustawi wa kiakili na kufikia malengo na ndoto zao kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.

Wanufaika: Watu binafsi, wanafunzi, vikundi, wafanyakazi, na jamii kiujumla wanaotaka kuboresha maisha yao kupitia vipaji walivyonavyo.
Faida za Huduma hii
  • Vipimo maalumu vya kisaikolojia ili kutambua vipaji na uwezo wako wa kipekee
  • Mwongozo wa jinsi ya kutumia vipaji vyako kwa mafanikio yako binafsi na jamii
  • Uelewa wa jinsi afya ya akili inavyoweza kuathiri uwezo wa kutumia kipaji/vipaji vyako
  • Mafunzo ya namna fikra chanya inavyoweza kukuza vipaji na ustawi wa akili
  • Kujengewa uwezo na kuimarishwa kimbinu (Mentorship and Coaching) ili kuboresha ufanisi na kuongeza tija kupitia vipaji vyako

Apple Star

Miradi
“Fanikisha Miradi yako kwa msaada wa mbinu za kisaikolojia”
Apple Star
Maelezo

Apple Star package inalenga kusaidia viongozi wa miradi na taasisi kupanga, kusimamia, na kuendesha miradi yenye mafanikio kupitia mbinu za kisaikolojia. Tunasaidia kuimarisha ustawi wa akili ili kuongeza ufanisi katika utawala wa miradi kwaajili ya maendeleo ya jamii na vizazi vijavyo.

Wanufaika: Viongozi wa miradi, taasisi, makampuni, vikundi vya kijamii, na mtu yeyote anayehusika katika usimamizi na utekelezaji wa miradi.
Faida za Huduma hii
  • Uelewa wa jinsi afya ya akili inavyoathiri usimamizi wa miradi
  • Mafunzo ya jinsi fikra ya Vizazi (generational mindset) inavyoweza kusaidia kufanikisha miradi
  • Ushauri wa jinsi magonjwa ya kisaikolojia yanaweza kuathiri utendaji wa miradi
  • Mbinu za kudhibiti msongo wa mawazo katika usimamizi wa miradi kwa ufanisi bora zaidi
  • Utapata vipimo vya kisaikolojia na matibabu kwa timu za miradi (project teams) ili kuongeza tija na ufanisi

Star Beauty

Uzuri Wangu
“Tambua uzuri wako wa ndani na nje kwa ustawi wako”
Star Beauty
Maelezo

Package hii inalenga kuwasaidia watu binafsi kuelewa na kuthamini uzuri wao wa kipekee. Tunatoa mwongozo wa kisaikolojia ili kuleta hamasa katika kujenga viwango binafsi vya uzuri wao, huku wakizingatia afya ya akili na ustawi wa vizazi vijavyo.

Wanufaika: Watu binafsi, wanafamilia, vijana, na mtu yeyote anayetaka kuboresha fikra na mtazamo wake kuhusu uzuri na ustawi wa akili.
Faida za Huduma hii
  • Uelewa wa jinsi uzuri unavyohusiana na afya ya akili na ustawi wa mtu binafsi
  • Vipimo vya kisaikolojia ili kusaidia kuthamini na kutambua uzuri wako binafsi
  • Ushauri wa namna ya kukabili changamoto za kisaikolojia zinazosababishwa na dhana potofu za uzuri/urembo
  • Mafunzo ya namna fikra chanya inavyosaidia kujenga thamani na hadhi yako binafsi
  • Mwongozo wa matumizi ya teknolojia na virutubisho vya lishe kusaidia uzuri na afya ya akili

Star Classic

Mentorship
“Jifunze kutoka kwa waliokutangulia, jenga ujuzi wako kwa ustawi wako”
Star Classic
Maelezo

Star Classic ni huduma zinazolenga kutoa msaada wa kisaikolojia kupitia programu za kujengewa uwezo zenye kulenga kukuza ujuzi na uwezo wa watu binafsi katika nyanja mbalimbali za kisaikolojia. Tunatoa mwongozo wa moja kwa moja kupitia ushauri wa kipekee kutoka kwa wazoefu na waliotangulia ili kusaidia ukuaji wako binafsi.

Wanufaika: Mtu binafsi, wanafunzi, wafanyakazi, vikundi, taasisi, na watu wote wanaohitaji msaada wa kisaikolojia kupitia programu za kujengewa uwezo ili kuboresha maisha na ustawi wa kiakili.
Faida za Huduma hii
  • Utapata ushauri na mwongozo wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu kulingana na taaluma yako
  • Mafunzo maalumu ya jinsi ya kufikia malengo yako binafsi
  • Vipimo na tathimini za kisaikolojia ili kusaidia kujenga mwelekeo sahihi wa ukuaji
  • Kujengewa uwezo maalumu kwaajili ya mabadiliko ya kifikra na ustawi wa kizazi chako na vizazi vijavyo

Rocket Star

Coaching
“Pata mwongozo sahihi, weka fikra zako kwenye njia ya mafanikio”
Rocket Star
Maelezo

Rocket Star package ni huduma zinazolenga kuwasaidia watu binafsi kupitia programu za kuimarishwa kimbinu (coaching) zinazojikita kwenye mbinu za kisaikolojia ili kuimarisha ustawi wa akili na kufikia malengo binafsi na ya kikazi pia. Programu zetu za kuimarishwa kimbinu huchangia kubadilisha fikra na kuongeza ufanisi kwa vizazi.

Wanufaika: Watu binafsi, wafanyakazi, wanafunzi, taasisi, makampuni, na mtu yeyote anayehitaji msaada wa kuimarishwa kimbinu (coaching) kwa ustawi wa akili na mafanikio yake binafsi.
Faida za Huduma hii
  • Mafunzo maalumu ya jinsi ya kutumia fikra chanya ili kuboresha ustawi wa akili na mafanikio yako
  • Mwongozo wa kisaikolojia kwa kutumia vipimo na tathimini za kina ili kufikia malengo binafsi na yale ya kikazi
  • Programu zetu zitakusaidia kuboresha uwezo wako wa kufanya maamuzi sahihi
  • Programu zetu zinazingatia ustawi wa vizazi na mafanikio endelevu

Furnance Star

Malezi
“Kuwa mzazi bora kwa ustawi wa watoto wako na vizazi vijavyo”
Furnance Star
Maelezo

Package hii inalenga kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wazazi ili kuimarisha mbinu bora za malezi. Tunatoa mwongozo na elimu ya kisaikolojia kwa wazazi ili kuhakikisha watoto wamelelewa katika mazingira yenye afya bora ya akili, hali ambayo husaidia ustawi wa kizazi hiki na vile vizazi vijavyo.

Wanufaika: Wazazi, walezi, familia, na vikundi vya jamii vinavyohusika na masuala ya malezi na ustawi wa watoto.
Faida za Huduma hii
  • Utapata elimu ya kina kuhusu athari za afya ya akili katika malezi
  • Utajifuza mbinu bora za kudhibiti msongo wa mawazo unaotokana na changamoto za malezi
  • Ushauri na tiba kwa magonjwa ya kisaikolojia yanayoathiri malezi bora
  • Utaelimika zaidi kuhusu saikolojia ya uchaguzi wa vifaa bora vya makuzi ya mtoto
  • Ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kukabiliana na changamoto za malezi kupitia tathimini za kisaikolojia
  • Mafunzo ya namna fikra ya vizazi (generational mindset) inavyoweza kuimarisha malezi bora na ustawi wa watoto

Star Overshine

Generational Mindset
“Jenga fikra za kizazi chenye ustawi kwa mafanikio ya leo na kesho”
Star Overshine
Maelezo

Package hii inajumuisha huduma zenye kulenga kusaidia watu na jamii kubadilisha fikra zao kwaajili ya ustawi wa kizazi chao na vizazi vijavyo. Tunatoa msaada wa kisaikolojia ili kuwasaidia watu kuboresha fikra zao juu ya kuacha alama katika kizazi chao, huku wakizingatia afya ya akili kwa maendeleo ya kudumu.

Wanufaika: Watu binafsi, familia, vikundi, taasisi za elimu, na jamii zinazohitaji kuboresha maisha yao na ya vizazi vyao kupitia mabadiliko ya kifikra (generational mindset).
Faida za Huduma hii
  • Utapata uelewa wa jinsi afya ya akili inavyoweza kuboresha fikra zako juu ya kizazi chako na vizazi baada yako
  • Utapata ushauri wa kisaikolojia ili kubadilisha fikra na kuimarisha ustawi wa vizazi
  • Utapata vipimo na tathimini za kisaikolojia ili kujua mwelekeo wa fikra zako na mchango wake kwa kizazi chako
  • Utapata mafunzo ya jinsi magonjwa ya kisaikolojia yanavyoweza kuathiri mawazo na fikra za kizazi, na njia bora za kuyakabili

Fantastic Star

Mama Mjamzito
“Jifunze namna bora ya kukabiliana na changamoto za ujauzito kwa ustawi wa afya yako na kizazi chako”
Fantastic Star
Maelezo

Fantastic Star ni Package inayojumuisha huduma zinazolenga kuwasaidia wanawake wajawazito kushughulikia changamoto za afya ya akili wakati wa ujauzito. Kwa kutumia mbinu za kisaikolojia, tunatoa msaada ili kuhakikisha wanawake wajawazito wanapata ustawi wa akili, kwa faida yao na kizazi wanachokileta duniani.

Wanufaika: Wanawake wajawazito, wazazi wapya, familia, taasisi za afya, vikundi vya wanawake, na familia zinazotarajia watoto hapo baadaye.
Faida za Huduma hii
  • Utapata uelewa wa jinsi afya ya akili inavyoathiri ujauzito na ustawi wa mtoto
  • Utanufaika na mafunzo ya jinsi ya kudhibiti msongo wa mawazo wakati wa ujauzito
  • Utapata msaada na elimu ya jinsi magonjwa ya kisaikolojia yanavyoweza kuathiri ujauzito na jinsi ya kuyakabili
  • Utapata vipimo na matibabu ya kisaikolojia kwaajili ya kuimarisha afya ya akili wakati wa ujauzito
  • Utajifunza namna ya kutumia fikra ya kizazi (generational mindset) katika kuhakikisha ujauzito unakuwa wenye mafanikio

Magic Star

Relaxation
“Pata utulivu wa akili na mwili kwa mafanikio yako na ustawi wa kizazi chako”
Magic Star
Maelezo

Magic Star ni Package maalumu ya kuwasaidia watu binafsi na makundi kutumia mbinu za kisaikolojia kupata utulivu, kupumzika, na kujitafakari kwa manufaa ya leo na kesho. Kupata utulivu na kupumzika ni muhimu kwa afya ya akili na mwili, na tunatoa mwongozo wa kisaikolojia kwaajili ya kupunguza na kukabiliana na msongo wa mawazo na kuongeza utulivu kwa ustawi wa maisha yako ya kila siku.

Wanufaika: Watu binafsi, wafanyakazi, wanafunzi, makundi ya kijamii, na watu wanaotaka kuboresha afya ya akili kupitia mbinu bora za utulivu na kupumzika.
Faida za Huduma hii
  • Utapata elimu ya kina kuhusu mbinu mbalimbali za utulivu na jinsi zinavyosaidia afya ya akili
  • Utapata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kuchagua mbinu sahihi za utulivu kwa maisha yako ya kila siku
  • Utapata elimu ya jinsi magonjwa ya kisaikolojia yanavyoathiri uwezo wako wa kupumzika na kupata utulivu
  • Utasaidiwa kufahamu namna fikra za vizazi zinaweza kuchangia katika utulivu wa akili na mwili
  • Utafahamu zaidi kuhusu saikolojia ya tiba ya mazingira na utalii

Special Star

Matibabu ya Muda Mrefu
“Huduma za matibabu ya muda mrefu kwa ustawi wa afya ya akili na maisha bora”
Special Star
Maelezo

Special Star ni package maalumu kwa watu wenye matatizo sugu au changamoto zinazohitaji matibabu ya muda mrefu. Tunatoa matibabu ya kina ya kisaikolojia, tathmini, na vipimo vya afya ya akili kwa wale wanaohitaji msaada wa muda mrefu ili kuhakikisha ustawi wa maisha yao ya kila siku.

Wanufaika: Watu binafsi wenye matatizo sugu, familia, vikundi vya msaada wa jamii, na watu wote wanaohitaji matibabu ya muda mrefu kwa afya ya akili na ustawi wa maisha yao.
Faida za Huduma hii
  • Utapata vipimo, tathmini na mwongozo thabiti juu ya tatizo lako na namna bora ya kuendana nalo kwa ustawi wako
  • Utanufaika na elimu ya jinsi afya ya akili inavyoathiri tiba za muda mrefu na ustawi wa kizazi chako na vizazi baada yako
  • Utapata matibabu ya muda mrefu ya kisaikolojia kwa matatizo sugu ya akili
  • Utapa mwongozo wa namna ya kutumia fikra ya vizazi (generational mindset) ili kuboresha matokeo ya matibabu ya muda mrefu

Star Touch

Matukio
“Ongeza thamani kwenye matukio yako kwa huduma bora za kisaikolojia”
Star Touch
Maelezo

Package hii inahusisha kuhudhuria na kushiriki katika matukio mbalimbali yaliyopangwa na wateja wetu. Lengo ni kutoa semina, mafunzo, warsha, na ushauri wa kisaikolojia kwa washiriki waliohudhuria wenye matukio husika. Kwa kufanya hivyo, tunachangia kuimarisha afya ya akili na ustawi wa washiriki na jamii kiujumla.

Wanufaika: Mashirika, taasisi, makampuni, vikundi vya jamii, waandaji wa matukio, na mtu yeyote anayetaka kuboresha na kunogesha matukio yake kwa huduma za kisaikolojia.
Faida za Huduma hii
  • Semina na mafunzo ya kina kuhusu masuala ya afya ya akili na jinsi ya kuyashughulikia
  • Ushauri wa kisaikolojia na vipimo kwa washiriki wa matukio husika ili kuboresha ustawi wao
  • Mafunzo ya jinsi magonjwa ya kisaikolojia yanavyoathiri mafanikio na maendeleo yetu kama jamii
  • Vitabu na vifaa mbalimbali vya afya ya akili vitakavyosaidia washiriki kufaidika zaidi na shughuli iliyoandaliwa

Wondrous Star

Psychological Application of Different Subjects
“Tumia Hisabati, Sayansi na masomo mengine kwa mtazamo wa kisaikolojia ili kuboresha maisha yako ya kila siku”
Wondrous Star
Maelezo

Wondrous Star Package hulenga kusaidia watu kuelewa na kutumia masomo ya darasani kama vile hesabu, kemia, fizikia, na baiolojia kwa mtazamo wa kisaikolojia katika maisha yao ya kila siku. Tunatoa mwongozo wa kipekee wa kisaikolojia wa jinsi maarifa haya yanaweza kutumika kusaidia ustawi wa akili na kushughulikia changamoto za maisha.

Wanufaika: Wanafunzi, walimu, taasisi za elimu, wafanyakazi, makampuni, na mtu yeyote anayevutiwa na kutumia sayansi na masomo mengine kuboresha maisha yao ya kila siku.
Faida za Huduma hii
  • Utapata elimu ya kipekee ya jinsi ya kutumia sayansi na masomo mengine kuboresha maisha yako
  • Utapata mbinu za jinsi ya kutumia maarifa ya hesabu, kemia, fizikia, baiolojia, na masomo mengine kutatua matatizo ya maisha ya kila siku
  • Utapata mafunzo ya jinsi fikra za vizazi zinaweza kusaidia katika kuunganisha elimu ya darasani na maisha ya kila siku
  • Matibabu na vipimo vya kisaikolojia vinavyohusisha matumizi ya sayansi katika kuboresha afya ya akili
Wasiliana Nasi
WhatsApp